Tarehe 3 Juni, Naibu Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Washauri la Bunge la Cambodia Bw. Chheang Vannarith ametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian amekutana na wageni. Wamezungumza kuhusu kuimarisha mawasiliano ya elimu na utamaduni na kuendeleza ushirikiano baina ya China na Cambodia.

Vannarith ametoa hotuba na kuzungumza na walimu na wanafunzi wa BFSU katika hali ya kirafiki.