Tarehe 3 Juni, Waziri wa Elimu, Sayansi na Vijana wa Georgia Bw. Givi Mikanadze, Balozi wa Georgia nchini China Bw. Paata Kalandadze, Naibu Waziri wa kwanza wa Elimu, Sayansi na Vijana wa Georgia Bw. Levan Ghirsiashvili wametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian amekutana na wageni. Mikanadze ametoa hotuba na kuzungumza na walimu na wanafunzi wa BFSU katika hali ya kirafiki.
