Mwanzo > Habari > Content

Kundi la Sanaa la BFSU Latembelea Ujerumani, Ubelgiji na Hungary

Updated: 2026-05-01

Tarehe 22 Aprili hadi Tarehe 1 Mei, kwa kutumwa na Kituo cha Ushirikiano na Mawasiliano ya Lugha kati ya China na Nchi za Nje cha Wizara ya Elimu ya China, Kundi la Sanaa la Chuo Kikuu cha BFSU limefanya ziara nchini Ujerumani, Ubelgiji na Hungary na kufanya maonesho ya sanaa, mihadhara na maonesho ya kitamaduni.

Shughuli hizo zimeonyesha umaalumu wa BFSU katika lugha na sanaa. Wachezaji wa BFSU wametembelea Taasisi ya Confucius ya Kitaaluma ya Göttingen nchini Ujerumani, Taasisi ya Confucius ya Liège nchini Ubelgiji, Kituo cha Utamaduni wa  Kichina mjini Brussels, na Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Eötvös Loránd nchini Hungary ili kuzidisha mawasiliano ya kitamaduni.


Baidu
map